Habari za usajili leo wakati Manchester United wameongezewa nafasi ya kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba baada ya wapinzani kujiondoa katika mbio za kuwania saini ya nyota Mfaransa mwenye thamani ya £100m.
25. N’Golo Kante – Leicester kwa Real Madrid
Real Madrid bado wanataka kumsajili kiungo wa Leicester City N’Golo Kante baada ya kujiondoka katika mbio ya kumsajili Paul Pogba. ( The Sun)
24. Borja Mayoral – Real Madrid kwa Wolfsburg
Wolfsburg bado wangali katika mazungumzo na Real Madrid kuhusu dili la kumsajili mshambuliaji Borja Mayoral kwa mkopo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo katika klabu hiyo ya Bundesliga Klaus Allofs.( ESPNFC)