Hapa tunaangalia vilabu vya soka vinavyokuwa na mashabiki wengi katika ulimwengu….Kwa mujibu wa utafiti. Mashabiki hao kwa ukweli hupenda klabu zao!

10.JuventusMilioni 22 za mashabiki duniani kote

Mabingwa wa Serie A mara nne, washiriki wa fainali ya Ligi ya Mabingwa katika msimu wa 2014/15. Ni klabu ya 10 katika soka kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni.

Juventus

9.Bayern Munich – Milioni 26 za mashabiki duniani kote

Mabingwa wa Bundesliga mara kadhaa ni klabu ya kwanza nchini Ujerumani na inakalia nafasi ya 9 duniani kwa hali ya kuwa na mashabiki wengi.

Bayern Fans

8.Inter Milan – Milioni 51 za wafuasi kwa ujumla

Vigogo wa San Siro walishinda vikombe vitatu mnamo 2010 wakifundishwa na Jose Mourinho. Timu hii haijashinda jambo hata moja tangu siku hiyo lakini idadi ya mashabiki wao hawapunguki kamwe na wanakalia nafasi ya 8 duniani.

Inter fans

7.Liverpool – Milioni 74 za mashabiki kwa ujumla

Liverpool inajulikana kama klabu yenye mashabiki wazee zaidi na waaminifu sana ulimwenguni kote. Bado wangali katika hali ya maadhimisho baada ya ushindi staajabu jijini Istanbul katika Ligi ya Mabingwa walipotoka nyuma na kushinda Ac Milan mnamo 2005. Wanashikilia nafasi ya saba katika hali ya mashabiki wengi duniani.

Liver Fans

6.AC Milan – Milioni 105 za mashabiki kwa ujumla

Klabu ya pili kwa mafanikio barani Ulaya ikiwa na vikombe 7 vya Ligi ya Mabingwa. Klabu ya San Siro walianguka katika miaka michache ipitayo tangu Carlo Ancelloti aiondoke. Lakini mashabiki wao wanaendelea kuwa thabiti na wanakalia nafasi ya sita ulimwenguni.

Milan fans